Mtu mmoja auawa na tembo wengine kadhaa kujeruhiwa mkoani Arusha. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Saturday, April 9, 2016

Mtu mmoja auawa na tembo wengine kadhaa kujeruhiwa mkoani Arusha.

Mtu mmoja ameuawa na tembo wengine kadhaa wamejeruhiwa katika  mapambano kati ya wananchi na kundi la tembo yaliyotokea katika  kijiji cha kitendeni kata ya Irkaswa tarafa ya Endyment wilayani  Longido mkoa  wa Arusha.
 
Mkuu wa Wilaya ya Longido Bw.Ernest Kahindi amesema katika  mapambano hayo pia tembo mmoja ameuawa na wengine sita  wamejeruhiwa na kwamba hali katika eneo hilo sio shwari na huenda  kukawa na madhara makubwa zaidi.
  
Akizungumza wakati anaelekea katika eneo la mapambano hayo yanayodaiwa kuanza mapema alfajiri Bw.kahindi amesema hatua za awali za kutuliza hali hiyo zilikuwa zinaendelea kwa ushirikano wa viongozi wa ngazi mbalimbali na watendaji wa idara za wanyamapori  zikiwemo za kuwaondoa tembo hao katika eneo hilo zoezi ambalo licha  ya  kuwa  gumu  lilikuwa linaendelea  vizuri.
 
Aidha Bw.Kahindi amesema tofauti kati ya tembo hao na wananchi ilijitokeza baada ya wanyama hao kumuua kijana mmoja wa jamii  ya kifugaji na ndipo wananchi hao wakajikusanya na kuanza kuwatafuta tembo hao na kuanza kupambana nao kutaka kulipiza kisasi  ambapo pia mwananchi mwingine mmoja amejeruhiwa vibaya na tembo zaidi ya sita pia wamejerihiwa vibaya kwa kuchomwa mikuki na  kupigwa kwa silaha zingine za jadi.
 
Hata hivyo Bw.Kahindi ambaye ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kuelekea eneo la tukio amesema taarifa  kamili ya tukio hilo na hatua zitakazochukuliwa itatolewa baadaye japo ameendelea kuwaomba wananchi kuepuka kuchukua sheria  mkononi ikiwemo ya kuamua kupambana na wanyama ili kuepusha madhara zaidi kutokea.
 
Asilimia kubwa ya eneo hilo ambalo ni mapito ya wanyama kwa muda mrefu sasa limekuwa katika hekaheka kati ya wananchi na  wanyama hao hasa unapotekea uharibifu ukiwemo wa wanyama kula mifugo ya wananchi ama kuua watu.
 
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin