Polisi,mkoani Simiyu yateketeza ekari 5 za bangi katika Pori la Akiba la Maswa. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Saturday, April 9, 2016

Polisi,mkoani Simiyu yateketeza ekari 5 za bangi katika Pori la Akiba la Maswa.


Jeshi la Polisi  mkoani  Simiyu limefyeka ekari tano za bangi na kuzichoma zaidi ya tani mbili ya bangi hiyo ambayo ilikuwa imekauka na tayari imeandaliwa kwa ajili ya kusafirishwa kwenda kuuzwa.
Akizungumza katika zoezi la opresheni ya ufyekaji wa bangi hiyo iliyofanyika katika kijiji cha Mwasenase kilichopo karibu na pori la Akiba la Maswa ,Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Simiyu,Kamshina Msaidizi wa Polisi ,Onesmo Lyanga amesema mashamba hayo ya bangi yamepatikana kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na kikosi cha intelijensia  ambacho kiliyagundua mashamba hayo.
 
Kamanda Lyanga ameonya wananchi wa kijiji hicho na vijiji vya jirani kuendelea kulima zao hilo ambalo ni haramu na badala yake wajikite katika kulima mazao halali  ambayo yatawapatia kipato kwani ardhi yao ni nzuri lakini badala ya kuitumia kulima mazao halali ya mahindi na mengineo wamegeuza kilimo cha bangi kama zao halali.
 
Aidha katika operesheni hiyo jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata nguo na vitu mbalimbali kama samaki ambavyo viliachwa na watu wanaosadikiwa kuwa majangili baada ya kuona askari ambapo inasemekana eneo hilo ndilo ambalo wamekuwa wakiandalia chakula kabla ya kuingia hifadhini kwenda kuwinda wanyama.
 
Opresheni hiyo ilishirikisha askari Polisi,askari mgambo na askari wa idara ya wanyama pori,ambapo kwa mjibu wa Kamanda Lyanga amesema operesheni hiyo itaendelea kutokana na jeshi hilo kubaini mashamba mengi ya bangi katika vijiji vingine.
 
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin