Siku
moja tu baada ya kuapishwa kuwa waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na
Uvuvi wa Zanzibar Mhe Hamad Rashid ameanza kazi kwa kishindo kwa kupiga
marufuku harakati za siasa wizarani na kuahidi hatosita kumwajibisha
mfanyakazi atakayeshindwa kutekeleza jukumu lake.
Mhe Hamad Rashid ambaye ni waziri kutoka chama cha upinzani ndani
ya seriklai ya CCM Zanzibar ametoa tahadhari hiyo huko Bungi mkoa wa
kusini Unguja aliposhiriki zoezi la upandaji miti la Zanzibar ambalo
linaendelea sehemu mbalimbali Unguja na Pemba huku ikiwa ni siku yake ya
kwanza kuanza kazi ambapo amesema sasa ni wakati wa kazi na sio siasa
anayetaka kujishugulisha na siasa aiache wizara huku akisisitiza
amepania kuona sekta hizo zake zinaleta mafanikio na mabadiliko.
Mhe Hamad Rashid amewataka wafanyaakzi wa wizara hiyo kuelewa
umuhimu wa wizara yao ambayo inachangia asilimia 75 ya ajira na asilimia
30 ya pato la serikali huku akiahidi kuwa mkweli na mchapa kazi lakini
hatokuwa na huruma kwa mfanyakazi ambaye haelewi jukumu lake la kuwepo
kazini, huku katibu mkuu wa wizara hiyo Affan Maalim amesema zoezi hilo
limekuwa la mafanikio makubwa ambapo linaendelea Unguja na Pemba.
Katika harakati hizo ITV ilifanikiwa kushinda na kupewa nafasi ya
kupanda miti wa Mdimu ambao ulipewa jina la ITV kutokana na chombo hicho
kuwa mstari wa mbele katika habari na kuhifadhi mazingira.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini