Mhandisi
wa maji katika halmashauri ya wilaya ya Rorya Bw Emmanuel Masanja,
amekamatwa na jeshi la polisi kwa amri ya mkuu wa wilaya hiyo baada ya
kutuhumiwa kuhusika na ubadhilifu wa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni
mia moja zilizolewa na ofisi ya waziri mkuu kwa ajili ya ukarabati wa
mradi wa maji katika mji mdogo wa Shirati wilayani humo.
Akizungumza baada ya Mhandisi huyo wa idara ya maji kukamatwa na
kukabidhiwa kwa jeshi la polisi na taasisisi ya kuzuia na kupambana na
rushwa nchini Takukuru wilayani Rorya, mkuu wa wilaya ya Rorya Bw Felix
Lyaniva, amesema baada mkuu wa mkoa kufanya ziara wilayani humo, uongozi
wa wilaya umebaini mkuu huyo wa idara ya maji kuhusika na ubadhilifu
huo wa kiasi hicho cha fedha na hivyo kusababisha wananchi wa mji wa
Shirati kukosa huduma ya maji kwa muda mrefu.
Katika ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali wilayani Rorya, mkuu
wa mkoa wa Mara Bw Magesa Mulongo, amesema lazima hatua za haraka
zikiwemo za uchunguzi zifanyike katika kuwezesha wahusika wote wa
ubadhilifu huo wanakamatwa na hatua kali zichukuliwe dhidi yao.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini