Mahakama
ya hakimu mkazi Kisutu Dar es Salaam imeamuachia huru aliyekuwa
mkurugenzi mkuu wa shirika la umeme nchini Tanesco William Mhando na mke
wake pamoja na waliokuwa maafisa watatu wa ngazi ya juu wa shirika hilo
la umeme nchini baada ya mahakama kuona hawana hatia.
Akisoma hukumu hiyo kwaniaba ya hakimu mkazi wa mahakama ya Kisutu
Kyey Lusema, hakimu wa mahakama hiyo Hellen Liwa amesema mahakama
imeamua kuwaachia huru watuhumiwa hao baada ya upande wa serikali
kushindwa kuithibitishia mahakama juu ya tuhuma zilizopelekwa mahakamani
hapo dhidi ya watuhumiwa hao.
Akisoma hukumu hiyo amesema upande wa serikali umeshindwa
kuthibitisha namna mhandisi William Mhando alivyotumia madaraka yake
vibaya ya ofisi kwa kuishawishi bodi ya Tanesco kuipa tenda ya kusambaza
vifaa vya Tanesco vyenye thamani ya shilingi miliioni 884.5 kampuni ya
Santa Clara ambayo inamilikiwa na mke wake, na kuitengenezea faida isiyo
halali kampuni hiyo ya zaidi ya shilingi milioni 31.
Ambapo kutokana na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo Mhando
hakuweza kutumia madarakaa yake vibaya kwani hakuhusika katika vikao vya
bodi vilivyotumika katika uidhinishwaji wa tenda hiyo kwa kampuni ya
Sanat Crala.
Katika hukumu hiyo hakimu Hellen amesema kitendo cha waendesha
mashitaka wa serikali kushindwa kuithibitishia mahakama kwa hutuma za
makosa sita yakiwemo ya kugushi nyaraka kwa bodi ya Tanesco inaifanya
mahakama kuwaachia huru watuhumiwa wote labda mpaka pale watakapokamatwa
kwa makosa mengine.
Maafisa hao wa juu wa zamani wa tanesco waliokuwa wakikabiliwa na
mashitaka hayo ni pamoja aliyekuwa mkurugenzi mkuu, wiliam mhando,
francis machalange (mhasibu mkuu tanesco), sophia misidai, na naftali
kisinga, ambaye ni ofisa ugavi wa shirika hilo.
Baada ya kusoma hukumu hiyo iliyokuwa fupi zaidi ya kesi hiyo
iliyofunguliwa na seriakli mapema may mwaka 2014, mawakili wa pande za
serikali na ile ya utetezi hawakuwa na lolote la kuzungumza, huku
mhandishi mhando akishindwa kuzungumza lolote na vyombo vya habari.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini