Afisa usalama feki wa Tanesco afikishwa Mahakamani mkoani Kagera. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Friday, April 15, 2016

Afisa usalama feki wa Tanesco afikishwa Mahakamani mkoani Kagera.


Jeshi la Polisi mkoani Kagera limemfikisha Mahakamani mkazi wa Manispaa ya Bukoba Anath Rutha maarufu kwa jina la nazimin kwa tuhuma ya kujifanya afisa usalama wa shirika la umeme (TANESCO) na tuhuma nyingine ya kumtishia kumuua meneja wa shirika hilo mkoani humo Hassan Saidi kwa maandishi ya ujumbe wa simu ya mkononi baada ya kufuatilia nyendo zake.
Mtuhumiwa huyo amefikishwa leo Mahakamani mbele ya Hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Bukoba,Charles Uisso huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la Polisi na Mashtaka yanayomkabili yamesomwa mbele ya Mahakama na Mwanasheria mkuu wa Serikali kanda ya Bukoba,Hashimu Ngole.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin