Waziri aagiza ng'ombe 6000 waachiwe huru. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Tuesday, February 2, 2016

Waziri aagiza ng'ombe 6000 waachiwe huru.

Waziri wa Mali asili na utalii Prof. Jumanne Maghembe amewataka askari wa kulinda wanyama pori katika hifadhi ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara kuwarudishia wananchi ng'ombe 6000 ambao walishikiliwa baada ya kuingia eneo la hifadhi eneo la Busega.
Waziri amefikia uamuzi huo baada ya Mbunge wa Jimbo la Busega CCM Dkt Rhaphael Chegeni ambaye ametaka kauli ya serikali kuhusiana na ng'ombe ambao wanazuiliwa katika hifadhi hiyo.
''Mheshimiwa naibu spika ngombe wamezuiliwa wakati wao hawana akili na wanateswa bila malisho je serikali inachukua hatua gani ili wananchi wachukue mifugo yao?'' Ameuliza Dkt. Chegeni
Akijibu swali hilo waziri Maghembe amesema ng'ombe hao waachiwe mara moja ili kuleta mahusiano mazuri kati ya wananchi wanaozunguka hifadhi pamoja na serikali.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin