Serikali ndiyo kikwazo kwa ajira nchini-Sakaya | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Tuesday, February 2, 2016

Serikali ndiyo kikwazo kwa ajira nchini-Sakaya



Mbunge wa Jimbo la Kaliua Mkoani Tabora Magdalena Sakaya CUF amesema kwamba tatizo kubwa la ajira nchi hii linachangiwa na serikali yenyewe.
Magdalena ameyasema hayo wakati akichangia mpango wa serikali kwa mwaka wa fedha 2016 &2017 ambao uliwasilishwa hapo juzi na wabunge kupewa nafasi ya kuchangia na kuishauri serikali kwa muda wa siku 5.
"Mheshimiwa Naibu Spika nchi hii ni tajiri sana tuna misitu ya kutosha lakini cha kushangaza tunakata miti tunasafirisha kwenda nje kwenda kutengeneza vifaa ambavyo tunakuja kuuziwa kwa bei ya juu wakati vijana nchini hawana ajira wanarandaranda mitaani". Alisema Sakaya
Pia akaongeza
"Serikali ndiyo chanzo cha kukosekana kwa ajira kwa vijana nchi hii maana hadi pamba za kusafisha masikio tunatoa nje, pia tumeifanya nchi hii kuwa nchi ya kupokea kila kitu wakati malighafi tunazalisha hapa hapa nchini,Serikali ifufue viwanda ili kuweza kuajiri maelfu ya vijana".
Aidha Mbunge huyo ameitaka serikali kutekeleza kwa vitendo miradi ya maji ambayo iliahidiwa katika wilaya ya Kaliua na kwa muda wote wa mpango uliopita vijiji vitatu tuu ndivyo viliweza kupewa kipaumbele.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin