Hatuwezi kuidharau Tanzania Prisons - Mwambusi | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Tuesday, February 2, 2016

Hatuwezi kuidharau Tanzania Prisons - Mwambusi


Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema watacheza kwa umakini na hawataidharau Prisons katika mchezo wa Mzunguko wa pili wa ligi kuu unaotarajiwa kuchezwa hapo kesho Uwanja wa Sokoine jijini mbeya.
Mwambusi amesema anaifahamu Prisons ni timu nzuri na watahakikisha wachezaji wao wanacheza kwa umakini ili waweze kuondoka na Pointi tatu.
Mwambusi amesema, mchezo huo ni muhimu kwao kushinda baada ya kufungwa 2-0 na Coastal Union na bado wanaamini kila mchezo ni fainali kwao ingawa wana kibarua kigumu cha kupata matokeo mazuri kwa wenyeji Tanznaia Prisons.
Mwambusi amesema, licha ya kumkosa beki wao Kelvin Yondani ana imani hakutakuwa na pengo kwani wamemwandaa mchezaji wa kucheza nafasi hiyo.
Yondani alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union ambako Yanga walifungwa ingawa inaongoza katika Msimamo wa Ligi hiyo kutokana na Pointi 39 sawa na Azam FC lakini zinatofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin