Wakizungumza mbele ya waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Mhe
Prof Makame Mbarawa wafanyakazi hao wamesema wamechoshwa na vitendo vya
unyanyasaji wanavyo fanyiwa na wakandarasi kutoka uchina huku wakilipwa
mishahara duni na kila wanaposhinikiza madai yao wanapuuzwa huku kukiwa
na mrundikano wa wafanyakazi kutoka uchina wanaofanya shughuli
wanazomudu wazawa na kuibua matabaka baina yao.
Kufuatia madai hayo meneja wa miradi ya barabara kutoka wizara ya
ujenzi, uchukuzi na mawasiliano deusdedit kakoko ameutaka uongozi wa
kampuni hiyo kuanza kutekeleza mara moja mambo ya msingi yanayohusu
ajira ikiwemo kutoa mshahara kulingana ujuzi wa mfanyakazi
ikilinganishwa na kima cha serikali pamoja na malipo ya likizo na muda
wa ziada.
Kwa upande wake waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Mhe Prof
Makame Mbarawa akitoa kauli ya serikali mara baada ya kusikiliza hoja za
pande zote mbili kuhusu mgogoro huo ameagiza kampuni hiyo na
wakandarasi wengine nchi nzima kuanza kutoa mikataba kwa wafanyazi na
ndani ya siku saba.
Waziri Mbarawa pia amekagua ujenzi unaoendelea wa barabara hiyo ya
Dodoma Babati ambayo ni sehemu iliyobakia bila kiwango cha lami kwenye
barabara kuu inayounganisha bara la Africa kuanzia Cairo Misri hadi Cape
town afrika ya kusini inayojulikana kwa jina maarufu la the great
north.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini