Waethiopia 83 walioingia nchini bila vibali wahukumiwa miaka mitatu jela na mahakama ya Iringa. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Monday, February 1, 2016

Waethiopia 83 walioingia nchini bila vibali wahukumiwa miaka mitatu jela na mahakama ya Iringa.



Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa imewahukumu kwenda jela miaka mitatu wahamiaji 83 raia wa Ethiopia walioingia nchini bila kibali huku pia ikiwahukumu jela miaka mitano dereva na utingo wa lori waliowasafirisha wahamiaji hao kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea nchini Malawi.
Akisoma hukumu hiyo mahakamani hapo hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu mkazi ya mkoa wa Iringa Mheshimiwa Edrew Scout amesema mahakama imezingatia maombi yote ya wahusika lakini kwakuwa biashara ya usafirishaji binaadam imezidi kushamili nchini mahakama imeona ni vema watuhumiwa hao wakatumikia adhabu ya kufungwa jela miaka mitatu au faini ya shilingi milioni moja na kurejeshwa kwao baada ya adhabu.
 
Mahakama hiyo imewakuta na hatia dereva na utingo wa lori lililowasafirisha wahamiaji hao Hance Mwakyoma na Alex Adam kwenda jela miaka mitano au faini ya shilingi milioni moja na nusu ambapo dereva wa lori Bwana Hance Mwakyoma amelipa faini hiyo na kuachiwa huru.
 
Katika kesi nyingine ya wahamiaji 12 raia wa Ethiopia waliokamatwa hivi karibuni wakiwa kwenye gari ya kusafirisha magazeti ya kampuni hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu makazi ya mkoa wa Iringa Richard Kasele amewahukumu kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya shilingi laki tano watuhumiwa hao huku kesi ya dereva wa gari lililowasafirisha pamoja na wasaidizi wake wawili ikiahirishwa hadi tarehe 15 mwezi huu.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin