Mto
mkubwa ambao chanzo chake bado hakijafahamika umelipuka katika ghala la
kuhifadhia mafuta ya kupikia lililopo eneo la Forest jijini Mbeya na
kuteketeza bidhaa zenye thamani ya mamilioni ya fedha.
Moto huo ambao umezuka majira ya saa 11 alfajiri umeteketeza sehemu
kubwa ya mafuta ya kupikia ambayo yalikuwa yamehifadhiwa ndani ya ghala
hilo kabla ya kudhibitiwa na vikosi vya jeshi la zimamoto kwa
kushirikiana na jeshi la polisi ambalo limelazimika kupeleka magari ya
kukabiliana na fujo kupambana na moto huo.
Baadhi ya wananchi ambao wameshuhudia moto huo wamelipongeza jeshi
la zimamoto kwa kuwahi eneo la tukio huku wakiwa na vifaa ambavyo
vimesaidia kuzima moto huo.
Akizungumza na ITV, mmiliki wa ghala hilo, Romanus Ng’wave amesema
anahisi chanzo cha moto huo kuwa ni hitlafu ya umeme kwa kuwa ndani ya
ghala hapakuwa na bidhaa zinazoweza kusababisha moto, huku kamanda wa
polisi mkoa wa Mbeya, Ahamed Msangi akizungumzia uamuzi wa kupeleka
magari maalum ya kukabiliana na fujo kupambana na moto huo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini