Mjadala
wa bunge kuhusu mpango wa maendeleo wa serikali umechukua sura nyingine
baada ya baadhi ya wabunge kutumia muda wao mwingi kuzungumzia mvutano
wa kisiasa unaoendelea sasa huko visiwani Zanzibar ambapo wamesema kuna
haja ya mgogoro huo kuangaliwa kwa jicho la karibu kwani unaweza
kukiingiza kisiwa hicho matatani.
Mjadala huo ulisasabisha mwanasheria mkuu wa serikali kuingilia kati ili kuleta utulivu.
Mbali na suala hilo la Zanzibar wabunge wengine walitoa maoni yao
kuhusu mpango uliowasishwa na waziri na kusema ambapo Mh Almas Maige
mbunge wa Tabora kasikazini amesema pango ulipwa kuipa nguvu sekta
binafsi kwa sabababu ndio muhimili mkuu wa uchumi.
Aidha Mh Abdalah Mtolea mbunge wa chama cha wananchi CUF amesema
inashangaza kuona kuwa ni zaidi ya miaka 50 sasa bado tatizo la maji Dar
es Salaam halijapatiwa ufumbuzi na mpango uliowasilishwa hautoi dira
kamili ambapo Mh Stepheni Ngonyani mbunge wa CCM amesema kabla ya
kutekeleza mpango huu serikali wamaliziye miradi ya mwanzo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini