Nchi za Tanzania na Msumbiji zatakiwa kutunza rasilimali ya mto Ruvuma. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Wednesday, February 3, 2016

Nchi za Tanzania na Msumbiji zatakiwa kutunza rasilimali ya mto Ruvuma.



Nchi za Tanzania na Msumbiji ambazo zinanufaika na mto Ruvuma unaomwaga maji yake bahari ya Hindi zimetakiwa kutunza rasilimali maji ya mto huo kwa maslahi ya nchi hizo mbili kwa kuwa rasilimali hiyo isipotumika vizuri na vyanzo vya maji vikaharibiwa huenda vita kuu ya tatu ya dunia ikawa ya kugombea maji.
Hayo yamesemwa na afisa wa maji bonde la Ruvuma na Pwani ya kusini Bw. Lazaro Msaru kwenye uzinduzi wa jumuiya ya watumia maji bonde la Dogo la mto Ruvuma (Juwamuru) uliofanyika Peramiho mjini Songea na kushirikisha wanajumuiya sabini wakiwemo watendaji wa kata na vijiji vya mpakani mwa Tanzania na Msumbiji nchi zinazotenganishwa na mto Ruvuma ambao una umuhimu mkubwa kwa nchi hizo mbili.
 
Katibu msaidizi wa jumuiya ya watumia maji bonde dogo la mto Ruvuma (Juwamuru) Bw. Andrea Mapunda amesema kuwa tayari vyanzo vya maji vimeshaharibiwa na jitihada za dhati zinatakiwa katika kuvitunza.
 
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Songea katibu tawala wa wilaya hiyo Bw. Juma Ally ametaka watumiaji wa maji wakubwa watambulike na kuwaagiza watendaji wa kata na viijiji kuwachukulia hatua za kisheria waharibifu wa vyanzo
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin