Breaking News..Kabwe Zitto Kununua Timu Kubwa ya Mpira Nchini.... | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Wednesday, February 3, 2016

Breaking News..Kabwe Zitto Kununua Timu Kubwa ya Mpira Nchini....

MBUNGE wa kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACT), ametangaza azma ya kuinunua timu ya soka ya JKT Kanembwa inayoshiriki LMBUNGE wa Kigoigi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.

Akizungumza , mbunge huyo alisema kuwa tayari ameshaanza mazungumzo na uongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mkoani Kigoma kuona kama upo uwezekano wa kuinunua timu hiyo.

Alisema kuwa mpango wa kuinunua timu hiyo unakuja katika kutekeleza azma ya kuwa na timu ambayo itacheza Ligi Kuu Tanzania Bara na kurudisha hadhi ya michezo ya mkoa Kigoma kwenye soka.zitto-kabwe-facebook-frontKabwe alisema kuwa iwapo uwezekano wa kuinunua timu hiyo utafanikiwa mpango utafanywa kuunda kampuni ambayo itakuwa ikisimamia uendeshaji wa timu hiyo kama ilivyo kwa timu ya Azam.

Alisema ni jambo la aibu kuona mkoa wa Kigoma hauna timu hata moja katika Ligi Kuu wakati sehemu kubwa ya wachezaji wanaochezea timu zinazoshiriki ligi hiyo wanatoka Kigoma.

Pamoja na azma hiyo alisema kuwa kama itashindikana kwa timu hiyo kununuliwa kutokana na taratibu za jeshi atatafuta timu nyingine ambayo ataisimamia na kuiwezesha kufanya vizuri ili iweze kucheza Ligi Kuu.

Katika kauli yake Kabwe ametanabaisha kuwa pamoja na mpango wa kuwa na timu ya mpira wa miguu, mpango wake ni kuhakikisha wachezaji wakongwe waliowahi kuchezea timu za madaraja ya juu na timu ya Taifa wakiwemo Juma Kaseja na wengine wanarudi mkoani humo ili kusimamia timu za mkoa huo na kuzifanya ziweze kucheza mashindano ya ligi mbalimbali nchini kwa mafanikio.

Kauli hiyo ya Zitto inakuja siku moja baada ya kuutangazia umma mazungumzo ya awali kati yake na Mkurugenzi wa timu ya Azam FC, Abubakar Bakhresa kuhusu kuanzisha shule ya kuendeleza vipaji Kigoma.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin