Serikali
imeombwa kufuatilia kwa karibu miradi yote wanayopewa wakandarasi
nchini kabla haijakabidhiwa kwakuwa imeonekana miradi mingi inajengwa
chini ya kiwango na kuisababishia serikali hasara kubwa huku wananchi
wakiendelea kubakia nyuma katika masuala mazima ya maendeleo.
Hayo yamesemwa na wananchi wa kata ya Kitangili mtaa wa Songambele
mkoani Shinyanga ambao wameamua kutumia wakati huu wa sikukuu za
kumaliza mwaka kusafisha mitaro na kuzibua makalavati katika barabara
zote za kata yao huku wakiitaka serikali kufuatilia kwa undani zabuni
wanazotoa kwa wakandarasi na kuhakikisha miradi inatekelezwa katika
viwango vinavyokusudiwa.
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo Bw.Hamis Omary amemlalamikia
mkandarasi aliyekuwa amepewa zabuni ya kujenga barabara yenye urefu wa
mita miambili kwa kiwango cha changarawe katika eneo la Somgambele na
kushindwa kukamilisha ujenzi huo huku mwenjekiti wa mtaa huo Bw.Leonard
Kaziba akiwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika
shughuli za maendeleo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini