Mpango huo umewasilishwa na waziri wa fedha na uchumi Mh Dk Philip
Mipango ambapo amesema sekta ya viwanda itapewa msisitizo mkubwa zaidi.
Wakichangia mpango huo baadhi ya wabunge wamesema umekuwa mzuri
japo yapo baadhia ya maeneo ambyo inaonekana serikali iliyasahau na
hivyo kuna haja ya kuuboresha zaidi ili uweze kuwa na tija.
Kwa upande mwingine baaadhi yao wamesema watendaji wa serikali
wanapaswa kuongeza kasi ili mipango iliyobainishwa iweze kutekelezwa
lakini kama haitakuwa na hivyo ni dhahiri kuwa mpango huo hautalisaidia
taifa.
Awali bungeni hapo kabla ya kuwasilishwa kwa hoja hiyo na Mh waziri
wa fedha kulitokea mvutano wa kikanuni na hatimaye kanuni zikatenguliwa
na bunge likakaa kama kamati ili kuweza kuijadili hoja hiyo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini