Tume
ya taifa ya uchaguzi nchini (NEC) imeanza zoezi la kufanya tathimini ya
uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana 2015 unaolenga kutambua mafanikio
na changamoto zilizojitokeza na kuanza kuzifanyia kazi zoezi
litakalofanyika katika kanda zote nchini likiwashirikisha wadau mbali
mbali zikiwemo asasi za kiraia.
Anakizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa tume hiyo jaji mstaafu
Damiani Lubuva, kamishna wa tume hiyo Prof Amoni Chaligha amesema
miongoni mwa mambo yanayofanyika ni pamoja na kuangali mchango wa wadau
mbalimbali wakiwemo wananchi katika kushiriki nakufanikiksha uuchaguzi
huo ukiwemo uliotolewa na asasi za kiraia zilizokuwa zimepewa jukumu la
kutoa elimu ya uraia.
Baadhi ya wawakilishi wa taasisi hizo za kiraia wamesema tatizo la
ukosefu wa elimu ya uraia na faida zake bado ni kubwa na wameitaka tume
kuhakikisha inakuwa ni agenda ya kitaifa na itolewe wakati wote badala
ya kusubiri wakati wa uchaguzi.
Hata hivyo wawakilishi wa baadhi ya makundi likiwemo la walemavu na
wazee wamesema bado hawajashirikishwa ipasavyo kutoa mchango wao na
wamesema asilimia kubwa ya wazee na walemavu wa kusikia walishindwa
kushiriki uchaguzi kutokana na kutowekewa miundombinu ya kuwawezesha
kusikiliza sera za wagombea wakiwemo wakalimani.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini