CUF msisue uchaguzi jipangeni - BAKWATA DSM | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Tuesday, February 2, 2016

CUF msisue uchaguzi jipangeni - BAKWATA DSM

Baraza kuu la Waislam mkoa wa Dar es salaam limeipongeza serikali ya awamu ya tano kwa jitihada mbalimbali inazofanya za kuimarisha nidhamu, kubana matumizi na kukuza uchumi.
BAKWATA Dar es salaam imetoa salamu hizo za pongezi leo lilipokutana na vyombo vya habari, na kusema kwamba hatua hizo zimeanza kuleta tija kwa taifa kama inavyoshuhudiwa pato la serikali linavyoongezeka,
“Kusudi kubwa la kuwaiteni leo ni kutaka kutoa salamu za pongezi kwa serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Mh. John Magufuli, kutokana na hatua mbali mbali inazozichukua zenye lengo la kuimarisha nidhamu hasa kwa watumishi wa umma, hatua mabazo zimeanza kuleta tija kubwa ka taifa letu kama wote hivi leo tunavyoweza kushuhudia jinsi pato la serikali likongezeka mwezi hadi mwezi”, alisema Sheikh alhadj Mussa Salum ambaye ndiye sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.
Pia Baraza hilo limeipongeza serikali kwa kitendo cha kubana matumizi na kuweka kipaumbele huduma za jamii, kama suala la elimu bure.
“Aidha tunaipongeza kwa dhamira yake ya kubana na kupunguza matumizi ya serikali, na badala yake kuelekeza fedha kwenye huduma za jamii na watanzania tumeshaanza kunufaika na huduma hizo kama vile suala la elimu bure”, alisema Sheikh Salum.
Vile vile Baraza hilo limeitaka serikali kushughulikia changamoto za jiji la Dar es salaam ikiwemo tatizo la foleni, kwani linazorotesha uchumi pale wafanyakazi wanapochelewa sehemu zao za kazi, na kuomba kuanza kutumika kwa mabasi ya mwendo kasi ili kupunguza tatizo hili.
Pamoja na hayo Baraza hilo limeongelea suala la Zanzibar huku likisema ninaunga mkono uamuzi wa ZEC, na kukiomba chama cha CUF kukubali kurudia uchaguzi, ili kutatua mgogoro huo.
“Kuhusiana na suala la mgogoro uliopo Zanzibar, sisi BAKWATA MKOA WA DAR ES SALAAM, tunaunga mkono uamuzi wa Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuamua kufanya uchaguzi wa marudio, hivyo basi naomba kuchukua fursa hii kukiomba chama cha Wananchi CUF ambacho kimeshatangaza kususia uchaguzi huo, viache kususia uchaguzi huo bali vijipange na kushiriki”, alisema Sheikh Salum.
sheikh Mussa Salum alipokuwa kwenye mkutano na wandishi wa habari (hawapo pichani
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin