Madereva daladala Mbeya wamegoma na kusababisha adha ya usafiri kwa abiria. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Tuesday, February 2, 2016

Madereva daladala Mbeya wamegoma na kusababisha adha ya usafiri kwa abiria.


Madereva daladala Mbeya wamegoma na kusababisha adha ya usafiri kwa abiria.
Wakazi wa jiji la Mbeya leo wamejikuta katika wakati mgumu kwa kukosa usafiri wa kuingia na kutoka katikati ya jiji baada ya madereva wa daladala zinazofanya safari zake kati ya Uyole na Stendi kuu kufanya mgomo ambao umeambatana na vurugu kubwa wakipinga njia wanazopita kwa madai kuwa ni mbovu, hali ambayo imesababisha jeshi la polisi kuingilia kati na kuwatawanya kwa mabomu ya machozi.
Madereva wa daladala zinazofanya safari zake kati ya Uyole, Isyesye na Ituha uelekea maeneo ya Majengo na Stendi kuu jijini Mbeya leo wamefanya mgomo ambao umeambatana na vurugu kubwa wakipinga kupita kwenye barabara kadhaa ambazo wamepangiwa na Sumatra kwa madai kuwa barabara hizo ni mbovu na hazina vituo vya kupakia na kushusha abiria.
 
Kutokana na vurugu hizo jeshi la polisi limeamua kuingilia kati kwa kuwatawanya madereva hao kwa mabomu ya machozi na akizungumzia mgomo huo, kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, kamishna msadizi mwandamizi wa jeshi la polisi, Ahamed Msangi amewataka wakazi wa jiji la Mbeya kuwa watulivu akisema kuwa hakuna sababu za kufanya fujo kwa sababu malalamiko ya madereva hao ni jambo linazozingumzika huku akidai kuwa anaamini kikao cha dharura ambacho kimeitishwa na mkuu wa mkoa wa Mbeya Abaas Kandoro kikihusisha wadau wote wa usafirishaji kitatoa ufumbuzi wa tatizo hilo.
 
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin