Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
limetengua kanuni ya 94 (1) ya kanuni za kudumu za bunge za mwaka 2006
ili kuliwezesha bunge kuweza kujadili mpango wa serikali utakaotaumika
kwa muda wa mwaka wa fedha 2016 & 2017.
Akitengua
kanuni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu katika
Serikali ya Awamu ya Tano, Jenista Mhagama amesema kwamba bunge
lilitakiwa likae kama kamati mwezi Nombemba ili liweze kujadili mpango
wa serikali lakini kutokana na uchaguzi mkuu uliokuwepo nchini kazi hiyo
ilishindikana.
Kwa msingi huo kutokana na uwezo wa bunge kupitia ibara ya 63 (3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayowezesha bunge kujadili mipango ya serikali,kwa muda muafaka serikali imeamua kutengua kanuni ili bunge likae kama kamati kwa muda wa siku 5 ili kujadili mpango wa serikali ili wabunge waweze kuishauri serikali kabla ya bunge la bajeti.
Aidha mpango huo ulishindwa kujadiliwa bungeni hapo juzi kutokana na kanuni za bunge kukiukwa kwa kusomwa bila kutengua kanuni ya 94(1).

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini