Nyumba 4,036 kujengwa kwa ajili ya askari Polisi | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Monday, February 1, 2016

Nyumba 4,036 kujengwa kwa ajili ya askari Polisi


Serikali imesema itajenga nyumba 4'036 na ofisi nchini kwa ajili ya askari polisi katika kipindi cha awamu ya kwanza hapa nchini katika mikoa 17.
Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa mambo ya ndani Hamadi Masauni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Momba Mkoani Mbeya David Silinde (CHADEMA) aliyetaka kujua mkakati wa serikali katika kutatua kero kuu ya askari polisi kukosa nyumba za kuishi pamoja na ofisi za kufanyia kazi.
''Mheshimiwa Spika Serikali inatambua uhaba mkubwa wa nyumba za watumishi wa nyumba za wafanyakazi wa wizara ya mambo ya ndani hasa askari polisi, ili kutatua tatizo hilo tumejipanga kupata mkopo kutoka benki ya Exim China ili kujenga nymba za polisi katika maeneo ambayo yana uhaba mkubwa zaidi nchini''. Amesisitiza Masauni.
Aidha Serikali imesema nyumba hizo zitahusisha pia upande wa Unguja na Pemba katika mgawanyo utakao kwenda kwa awamu mbalimbali.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin