Umoja wa makanisa umechukua hatua ya kukemea usafirishaji haramu wa
buinadamu kutokana na mkoa wa Ruvuma kutajwa kushika nafasi ya tatu
nchini kwa biashara hiyo ambapo katibu wa wanawake wa umoja wa makanisa
mkoa wa Ruvuma Mwalimu Imelda Mbawala anasema kuwa wanaosafirishjwa kwa
biashara hiyo ulaghaiwa kutafutiwa kazi ughaibuni wakishafika huo
hunyang’anywa pasport zao za kusafiria na mawasiliano yao huzuiwa.
Akihubiri katika ibada iliyofanyika katika kanisa la kiinjili la
kiluhteri (KKKT)dayosisi ya Ruvuma askofu wa kanisa hilo askofu Amon
Mwenda amepinga biashara ya usafirishaji wa binadamu kama bidhaa huku
akiwahimiza waumini kupendana wao kwa wao ambapo padre wa kanisa
katoliki padre Turdo Chuma ameyataka makanisa ya kiafrika kukataa ndoa
za jinsia moja kwa kuwa si utamaduni wao.
Ibada hiyo iliendana na maombi ya kuliombea taifa amani na kumwomba
mungu kukomesha ugaidi na biashara haramu ya binadamu yaliyoongozwa na
wanamaombi kumi toka makanisa kumi ya umoja wa makanisa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini