Wawindaji haramu wamuua rubani nchini Tz., | nyula blog

nyula blog

Habari Kila Pande

  • HOME
  • MAGAZETI
  • AJIRA
  • PICHA
  • MATUKIO
  • SIASA
  • ELIMU
Breaking News
Loading...

Sunday, January 31, 2016

Wawindaji haramu wamuua rubani nchini Tz.,

Published Under KITAIFA MATUKIO

Wawindaji haramu nchini Tanzania wamuua rubani Muingereza
Shirika moja la wakfu wa utunzaji wa mazingira, linasema kuwa rubani mmoja raia wa Uingereza, amepigwa risasi na kuuawa nchini Tanzania.
Rubani huyo anasemekana kuwa alikuwa akipepeleza mzoga wa ndovu porini alipodunguliwa na mwindaji haramu aliyekuwa amejificha .
Operesheni hiyo ilikuwa katika mbuga ya wanyama pori ya Maswa Kaskazini mwa Tanzania.
Shirika hilo lenye makao yake nchini Marekani- The Friedkin Conservation Fund, linasema kuwa rubani Roger Gower, alikuwa akiwasaidia utawala nchini Tanzania kukabiliana na wawindaji haramu katika maeneo ya Serengeti, aliposhambulia .
Maafisa wakuu wa serikali ya Tanzania, wanasema kwamba bwana Gower alifaulu kutua helikopta hiyo lakini akafariki muda mfupi baadaye kutokana na majeraha ya risasi.
 
Wawindaji haramu wamuua rubani nchini Tz
Hadi sasa hakuna aliyekamatwa kwa mauaji hayo.
Inaaminika kuwa mvamizi alikuwa na bunduki yenye uwezo mkubwa kwani iliweza kupenya ubavu wa ndege hiyo na kumjeruhi marehemu.
Familia ya marehemu inatarajiwa nchini Tanzania hii leo kuandaa mipango ya maziko.
Hivi karibuni, utawala nchini Tanzania umekuwa ukikosolewa kwa kushindwa kutoa maelezo ya kina kuhusiana na uwindaji haramu wa pembe za ndovu.
Uwindaji haramu umeenea sana katika pori ya Maswa na sio tukio la kwanza ambapo wanaharakati wanaolinda wanyama wa porini wanashambuliwa na wawindaji haramu.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

facebook

twitter

Tweet

google+

linkedin

Total Pageviews

Popular Post

  • matokeo ya kidato cha nne 2015 /2016
    S3911 UKUNJWI S3912 KIBURUBUTU S3913 KIVESA S3914 ALFAGEMS S3915 CHIKONJI S3916 MANG'ONYI...
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO AWAMU YA PILI (SECOND SELECTION) KWA MWAKA 2016
    Tumia namba ya shule, jina la mwanafunzi au shule atokayo kurahisisha kupata shule aliyochaguliwa mwanafunzi ...
  • QT 2015 RESULTS FOR : M0104 - BWIRU BOYS SECONDARY SCHOOL CENTRE
    February 17, 2016    NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA             Page : 1                  QT 2015 RESULTS FOR : M0104 - BWI...
  • Ambari Nyeupe Ni Tiba Ya Kuongeza Ukubwa Wa Maumbile Ya Kiume Yaliyo Sinyaa.
    Ipo  idadi  kubwa  ya  wanaume  wanao  kabiliwa na  changamoto  ya  kuwa  na  maumbile  madogo  ...
  • Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Novemba 5
  • AJIRA ZATANGAZWA.
    TANZANIA ELECTRICAL SUPPLY COMPANY LIMITED TANESCO EMPLOYMENT OPPORTUNITITIES EXTERNAL ADVERTISEMENT LABORATORY TECHNICIAN (1 POST)...
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI KWA MWAKA 2016
    Tumia namba ya shule, jina la mwanafunzi au shule atokayo kurahisisha kupata shule aliyochaguliwa mwanafunzi ...
  • Angalia thamani yako, yanini kumng’ang’ania asiyekupenda?
    Ili mapenzi yaweze kuwa bora kwa kila aliye katika mahusiano, huwa ni vyema kila mmoja kuiona thamani ya mwenzake. Ukipenda kujiang...
  • Wabunge wa Upinzani Kuanza Vikao vya Kutafuta Suluhu na Naibu Spika
    Kambi rasmi ya upinzani imepanga kufanya vikao vya kujadili suluhu ya kudumu ya mgogoro na Naibu ...
  • Tanzania Nchi nzuri.

Blog Archive



My Blog List

  • nyula blog
    Kwema watu wangu
  • Kurasa Mpya
    MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA ECKERNFORD UNIVERSITY TANGA -DEGREE 2016/2017
  • categories
    ORODHA YA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI KWA MWAKA 2016
  • utamuwetu
    TUSHEREKEE PAMOJA.
  • Yuvinusm
    New Video: Cindy & Wahu – Yeye
 
Copyright © , nyula blog. All rights reserved. Designed By - Yuvinusm | Mini Habari