Muungano wa Afrika AU hautatuma kikosi cha walinda amani hadi pale serikali ya rais Pierre Nkurunziza itakapotoa mwaliko.
Msemaji
wa Muungano wa Afrika AU, amesema kuwa umoja huo hautatuma majeshi ya
kulinda amani nchini humo hadi pale watakapopokea mwaliko kutoka kwa
taifa hilo la kanda ya Afrika Mashariki.Kauli hiyo ni kinyume na pendekezo la awali la umoja huo ambao uliibua taharuki kuhusu uhalali wake na wajibu wake wa kulinda maisha ya wananchi.
Mjumbe maalum wa umoja huo kanda ya maziwa makuu Ibrahima Fall, anasema kuwa haijawahi kuwa nia ya AU kutuma walinda amani, bila ya idhini ya taifa husika.
- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, aliwaambia viongozi wa Afrika kwamba anaunga mkono pendekezo lao la kutuma askari 5,000 wa kuweka amani huko Burundi.
Machafuko nchini humo yalitibuka baada ya Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania uchaguzi katika muhula wake wa tatu.
Wapinzani wake walisema Nkurunziza alikuwa anakiuka katiba ya taifa na kisha maandamano yakaanza kukotokea hata jaribio la mapinduzi ambayo ilizimwa na kisha rais huyo akaibuka mshindi katika uchaguzi ambao ulisusiwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa wa upinzani.
Kulikuwa na pendekezo la kutuma kikosi cha wapiganaji 5,000 wa muungano wa Afrika ilikuokoa maisha ya wapinzani wa rais huyo.
Awali rais Nkurunziza alionya kuwa majeshi yake yangewakabili vikali jeshi hilo ''Vamizi'' akisema kuwa nchi hiyo iko salama na kuwa ni vitongoji vichache tu vya Bujumbura ambavyo ni ngome ya upinzanani.
Kauli ya mwaka jana wa Nkurunziza kuamua kuwania urais kwa muhula wa tatu ilisababisha vurugu nchini humo, ambapo mamia ya watu wameuwawa na wengine wengi wakitorokea mataifa jirani.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini