WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema suala la ada
elekezi linaendelea kufanyiwa kazi na serikali na likifika hatua nzuri
litahusisha wadau wote ili kupata maoni yao.
Ametoa
ahadi hiyo leo mchana (Jumapili, Januari 31, 2016) wakati akizungumza
na mamia ya waumini walioshiriki ibada ya kumuingiza kazini Mkuu Mpya wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Fredrick
Onaeli Shoo iliyofanyika kwenye usharika wa Moshi Mjini, Dayosisi ya
Kaskazini.
Waziri Mkuu Majaliwa ambaye alihudhuria ibada hiyo kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli alikuwa akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa na Dk. Shoo ambaye alisema kama serikali inataka kuondoa ada elekezi haina budi kuziimarisha shule zake ili ziwe kama zilivyokuwa zamani.
Akijibu hoja kuhusu miundombinu ya reli, Waziri Mkuu alisema serikali imeamua kufufua miundombinu hiyo na kwamba hivi sasa inafanya mapitio ili kujua gharama halisi kwa maeneo husika. Alisema Serikali imepanga kuanza na maeneo manne ambapo la kwanza alilitaja kuwa ni reli ya kutoka Dar es Salaam – Mwanza – Tabora – Kaliua – Mpanda hadi Karema.
“Eneo la pili ni reli ya ukanda wa Kaskazini ambayo itatoka Dar es Salaam – Tanga – Arusha hadi Musoma. Ya tatu ni ya kutoka Tabora – Kahama – Kigali (Rwanda) na kuishia nchini Burundi ambayo tunataka isaidie kusafirisha mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam. Reli ya nne ni ile ya kutoka Mtwara kupitia Tunduru kwenda Songea hadi Mbamba Bay,” alisema.
Kuhusu ulinzi wa demokrasia ndani ya Bunge, Waziri Mkuu alisema anakubaliana na Askofu Dk. Shoo juu ya mihimili yote mitatu kuheshimiana na kwamba ameshukuru kwamba ameonya juu ya lugha zinazotumika ndani ya Bunge.
“Bunge ni eneo linaloweza kujenga jamii mpya kwa sababu Bunge ni kioo na jamii ya watanzania inatuangalia sisi tuliomo mle. Ni vema tuwe na lugha nzuri, tabia njema na hata jinsi tunavyovaa ili wanaotuona wapate hamu ya kuiga,” alisema.
Kuhusu ombi la kuibuliwa upya mchakato wa Katiba mpya, Waziri Mkuu alisema suala hilo amelichukua na anaenda kulifanyia kazi. “Nakuhakikishia Baba Askofu ushauri ulioutoa kwa serikali tumeupokea,” alisisitiza.
Mapema, akitoa hotuba yake, Askofu Mkuu Dk. Shoo alisema Bunge ni nyumba ya demokrasia kwa hiyo jamii inatarajia kuona hoja zikijadiliwa kwa haki na amani badala kutumia ubabe na mabavu au nguvu ya dola.
“Nimewaona baadhi ya wabunge mko hapa… hili ninalolisema ni lenu na linawahusu ninyi na spika wenu. Wabunge tunzeni heshima yenu na Mungu awasaidie kulitimiza hilo. Wewe Waziri Mkuu ni Msimamizi wa shughuli za serikali bungeni kwa hiyo una kazi ya kusimamia. Kila mhimili unapaswa utunze heshima yake…,” alisisitiza.
Kuhusu Katiba mpya, Askofu Dk. Shoo alisema watanzania wengi wana kiu ya kuona mchakato huo ukiibuliwa upya na kukamilishwa ili nchi ipate Katiba mpya yenye kukidhi kiu ya watu wake na inayoheshimu matakwa ya wengi.
“Mchakato huo ukianza utumike kuganga majeraha yote yaliyopita. Tukifanya hivyo tutakuwa tumeisaidia Serikali ya Awamu ya Tano kuipelekea nchi yetu kule ambako imedhamiria. Yote yanawezekana tukitaka na tukipenda,” alisisitiza.

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini