Wahamiaji wengi hufanya safari hatari kuingia Ulaya
Takriban wahamiaji 42 wanaripotiwa kuzama baharini kwenye visa viwili katika bahari ya Aegean.
Mashua moja ilizama nje ya kisiwa kidogo cha Kalolimnos na kuwaua watu 34 wakiwemo watoto 11.Watu wengine wanane walikufa baada ya mashua yao kuzama nje ya kisiwa cha Farmakonisi.
Chansela wa Ujerumani Angela Merkel hii leo anakutana na waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu mjini Berlin kuzungumzia suala hilo.
Siku wa Alhamis waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls alionya kuwa tatizo la uhamiaji barani ulaya linaiweka ulaya hatarini.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini