Zaidi ya Nyumba 1400 zimebomoka katika wilaya ya kilosa, mkoani Morogoro, huku kaya 1840 zenye jumla ya wakazi 8091 zikokosa mahali pa kuishi baada ya kukumbwa na mafuriko ya mvua iliyonyesha wilayani humo.
Hatua hiyo inapelekea wakazi wa wilaya hiyo kupaza sauti kwa taasisi mbalimbali za watu binafsi na serikali nchini kuendelea kujitokeza kwa wingi kuwasaidia kwani hali yao bado sio nzuri kiuchumi.
Wilaya ya Kilosa ni moja wapo ya wilaya ambayo imekuwa ikumbwa na janga la mafuriko ya mara kwa mara, hatua inayopelekea wakazi wa mji huo kuishi kwa shida kutokana na kukosa makazi pamoja na chakula.
Afisa Mtendaji Kata ya Magomeni mkoani humo Bw Godson Chiduli ameziomba Taasisi mbalimbali zinazopatikana mkoani hapo kuunga mkono jitihada za serikali kwa kujitokeza kuwasaidia wananchi hao walioathirka na mafurika hayo yaliyotokea hivi karibuni.
katika kata ya Magomeni Wilayani Kilosa mvua iliyonyesha kwa muda mfupi iliweza kuleta kilio kwa wananchi wa kata hiyo hatau iliyopelekea wakazi hao kuhamia katika majengo ya shule kwa ajili ya kujihifadhi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini