Tanzania inaripotiwa kupunguza matukio ya uhalifu ya mitandao kwa asilimia 60, ikiwa ni miezi mitano tangu kuanza kutumika kwa sheria ya makosa ya aina hiyo nchini.
Hata hivyo, bado inaelezwa kuongezeka kwa changamoto za kimtandao kutokana na kasi ya ukuaji wa matumizi yake, hatua ambayo mara nyingine inatajwa kuwa kikwazo kwenye utekelezaji wake.
April Mosi 2015, Bunge la Tanzania lilipitisha Sheria ya Makosa ya Uhalifu wa Mtandao na Sheria ya Miamala ya Kielektroniki, lengo likiwa ni kukabiliana na makosa hayo yaliyokuwa yakiongezeka kwa kasi.
Baadhi ya makosa hayo ni wizi wa fedha kwa njia ya mitandao, udukuzi wa taarifa, picha za ngono za watoto na kuingilia mifumo ya kompyuta kinyume cha sheria na uchochezi.
Pamoja na kupungua kwa makosa hayo, wataalamu wa masuala hayo bado wanakutana kujadili mbinu zaidi za kukabili changamoto mpya, zinazoendelea kuwa kikwazo kwenye utekelezaji wa sheria hiyo.
Hata hivyo, utekelezaji wa sheria hiyo ulipokelewa kwa hisia tofauti na Watanzania, baadhi yao wakidai ilikuwa sheria kandamizi iliyolenga kubinya uhuru wa taarifa, hatua inayowasukuma wataalamu kuendelea kutafuta njia bora ya kuielimisha jamii kuhusu matumiza ya sheria hiyo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini