Maafisa wa polisi Mjini Mogadishu wameripoti kuwa Bomu lililotegwa ndani ya gari limelipuka nje ya mgahawa mmoja uliopo katika ufukwe wa bahari katika mji mkuu wa Somalia .
Masuhuda
wamesema kuwa gari hilo lililojaa vilipuzi liligonga mgahawa huo
maarufu wa Lido Beach kabla ya watu watano kujitokeza na kuanza kufyatua
risasi.
Lido beach ni moja ya Mgahawa uliopo pembezoni mwa Mogadishu na huwavutia maelfu ya vijana wa Somalia kwenda kujipumzisha na kujifurahisha.
Jeshi la polisi kupitia kwa Meja Abdiqadir Ali limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na bado haijajulikana kama kuna waliojeruhiwa na shambulizi hilo, pia uchunguzi bado unaendelea kuwabaini waliohusika.
Chanzo BBC

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini