Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Magufuli amemteua Luteni
Jenerali Venance Mabeyo kuwa mnadhimu mkuu wa majeshi ya ulinzi sambamba
na kumuongezea muda wa mwaka mmoja Jenerali Davis Mwamunyange kuendelea
kuwa mkuu wa majeshi hayo ya ulinzi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mkuu wa
majeshi ya ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange amesema mbali ya uteuzi na
uongezaji muda wa nyadhifa hizo za juu kabisa za majeshi ya ulinzi
nchini, rais Dr.Magufuli pia amewateua maafisa wengine nane wa JWTZ
kushika nyadhifa mbalimbali za juu ndani ya jeshi hilo.
Wengine walioteliwa kushika nafasi hizo ni meja Jenerali James
Mwakibolwa kuwa mkuu wa kamandi ya jeshi la nchi kavu, meja Jenerali
Yakub Sirakwi kuwa mkuu wa chuo cha ulinzi cha taifa, Brigedia Jenerali
George Ingram kuwa mkuu wa kamandi ya anga.
Mbali ya hao Brigedia Jen.M.Wisamuhyo kuwa mkuu wa JKT,
Brig.Jen.Jacob Kingu kuwa mkuu shirika la mizinga, Brig.Jenrobison
Mwanjela ameteuliwa kuwa mkuu wa chuo cha tiba Lugalo, Brigedia
Jen.George Msongole kuwa mkuu wa kamanda ya Tembo na Brige.Jen.Sylvesta
Minja kuwa mkuu wa chuo cha ukamanda na unadhimu.
Wateule hao wa nyadhifa hizo jeshini wameziba nafasi za waliokuwemo
ambao wamestaafu baada ya muda wao wa utumishini jeshini kufikia tamati
kasoro meja Jeneral Sirakwi ambaye anaziba pengo la meja Jen.Gaudence
Milanzi aliyeteuliwa kuwa katibu mkuu wa wizara ya mali asili na utalii.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini