Shirika
la ugavi wa umeme Tanzania (Tanesco) mkoa wa Ruvuma limemnasa mtu
anayelihujumu shirika hilo aliyetajwa kwa jina la Leginald Komba mkazi
wa Makambi mjini Songea mkoani humo ambaye anatuhumiwa kwa kuchezea mita
ya Tanesco ili atumie umeme kidogo na kulipia kidogo tofauti na
alivyotumia.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo Bw. Leginald Komba anayekadiriwa kuwa na
umri wa miaka arobaini na tano na hamsini na anatembelea magongo
alifanikiwa kutoroka nyumbani kwake akiwa mikononi mwa polisi na maofisa
wa Tanesco baada ya kuwaomba akanywe dawa na aliporuhusiwa alitorokea
kusikojulikana na bado anasakwa na polisi kwa kulihujumu shirika la
Tanesco.
Naye mwenyekiti wa mtaa wa Makambi manispaa ya Songea mkoani Ruvuma
kulikotokea hujuma hiyo Bw. Anwar Nyoni anawatahadharisha wananchi wake
kuhusiana na kulihujumu shirika la Tanesco.
Mkaguzi wa mita mkoa wa Ruvuma Bw. Hamis Kibona anasema kuwa pamoja
na kuchukuliwa hatua za kisheria na kutakiwa kulipa fidia mhujumu wa
Tanesco anakatiwa huduma ya umeme.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini