Nani mfisadi zaidi Kenya? | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Tuesday, January 26, 2016

Nani mfisadi zaidi Kenya?

Mutunga

 
, Jaji Mkuu Mutunga alisema Kenya imeshikwa mateka na 'magenge ya wanyang'anyi'
Nani mfisadi zaidi Kenya? Ndilo swali ambalo limejitokeza baada ya viongozi wawili wakuu wa Bunge na Mahakama kujibizana mtandaoni.
Chanzo cha majibizano haya ni taarifa ambayo Jaji Mkuu Dkt Willy Mutunga aliitoa akitangaza kwamba alikuwa amepotea habari za madai ya ufisadi dhidi ya jaji mmoja wa Mahakama ya Juu.
Jaji huyo anatuhumiwa kupokea hongo ya $2 milioni ili kupendelea upande mmoja kwenye kesi ya uchaguzi.
Dkt Mutunga alisema uchunguzi ulifanywa na kikao maalum cha Tume ya Huduma za Mahakama (JSC) kingeandaliwa Jumatano kujadili matokeo ya uchunguzi huo.
Kiongozi wa Wengi Bungeni, Bw Aden Duale, ambaye ndiye anayewakilisha serikali Bungeni, akichangia kwenye taarifa hiyo aliandika: “Sasa Jaji Mkuu amethibitisha kwamba idara ya mahakama na mahakama ya juu hasa, imejaa ufisadi.”
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin