ZITO Kabwe Awashukia Takururu Juu ya kashifa ya Lake Oil na IPTL . | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Wednesday, January 27, 2016

ZITO Kabwe Awashukia Takururu Juu ya kashifa ya Lake Oil na IPTL .

Zitto Kabwe
IKIWA imepita siku moja toka taasisi ya kupambana na Rushwa TAKUKURU kupitia kwa naibu mkurugenzi mkuu wake Valentino Mlowola kutangaza kuwa hadi kufikia sasa taasisi hiyo imefikisha mahakamani jumla ya kesi 36,Mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe ameijia juu taasisi  hiyo kwa kushindwa kuichukulia hatua kampuni ya mafuta ya Like Oil ambayo inatuhumiwa kukwepa kodi.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Zitto ameandika hivi.

"Nimesoma taarifa ya ‪#‎TAKUKURU‬ kuhusu kesi zaidi ya 30 na mashauri 4 mazito yanayopelekwa mahakamani hivi karibuni. LakeOil anatuhumiwa kukwepa kodi tshs 8 bilioni na kupewa miezi 2 walipe. IPTL/PAP inalipwa kila mwezi 8 bilioni na #TAKUKURU wameufyata kueleza umma hatua wanazochukua. Miezi 3 sasa toka Magufuli aingie madarakani, Harbinder Singh Seth keshavuta tshs 24 bilioni. Kama kawaida tunaanza kuona PR work ya vipaza sauti wa IPTL/PAP wakipewa kurasa za mbele za magazeti makubwa na yenye heshima nchini. Usaha wa jipu la IPTL unanuka.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin