Shirikisho la Wafanyakazi nchini Tanzania
(TUCTA),limetiaka serikali kuongeza juhudi katika upekuzi wa viwandani
na sehemu nyinginezo za uzalishaji kwa kuwa wageni wengi wasio na vibali
inasemakana wanafanya kazi huko.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi, Nicolas Mgaya
Akizungumza
na Waandishi wa Habari jana Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa
Shirikisho la Wafanyakazi, Nicolas Mgaya amesema wamebaini wageni wengi
wanfanya kazi kwa kujificha katika viwanda mbalimbali nchini kwa kufanya
kazi mchana na kutoka usiku.
Mgaya amesema ili fursa za ajira ziongezeke nchini serikali haina budi kupita kiwanda kwa kiwanda nyumba kwa nyumba ili kuwabaini wafanyakazi raia wa Kigeni wanaofanya kazi kinyume cha sheria.
Aidha Mgaya ameongeza kuwa kwa sekta nyingi za uzalishaji ikiwemo na mahoteli zimevamia na rais wa kigeni kutoka nchi jirani na kufanya shughuli ambazo hata watanzania wengine wa kawaida wana uwezo wa kuzifanya.

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini