Askofu
Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Kardinali Polycarp
Pengo aliyekuwa amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete,
Muhimbili ameruhusiwa baada ya afya yake kuimarika.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Profesa Mohammed Janabi alisema jana kuwa Kardinali Pengo aliruhusiwa saa 6.30.
Awali,
Profesa Janabi alisema Kardinali Pengo alilazwa katika kitengo hicho
mwaka jana kabla ya kuruhusiwa siku 10 baadaye baada ya kupata nafuu na
alipewa siku tisa kurudi hospitalini hapo kwa ajili ya kuendelea
kufuatilia zaidi afya yake.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini