Asilimia
96 ya watanania wanamkubali Rais Magufuli, na asilimia 88 ya wananchi
Tanzania wameonesha imani ya kuwa Rais Magufuli ataendelea na kasi
aliyoanza nayo katika uwajibikaji.
Wananchi
hao pia wamevutiwa na uondoaji wa wafanyakazi hewa, utoaji wa elimu
bure pamoja na usimamishaji watumishi wa serikali kwa makosa mbalimbali.
Takwimu zilizotolewa kwa vyombo vya habari na shirika la TWAWEZA jana
jijini Dar es salaam kupitia kwa mkurugenzi mtendaji wa wa shirika hilo
Aidan Eyakuze, zimebainisha kuwa asilimia 69 ya watanzania
wamefurahishwa na uondoaji wa wafanyakazi hewa uliotajwa, asilimia 67
wamefurahishwa na elimu bure huku asilimia 61 wakipendezwa na utumbuaji
majipu.
“Kwa
ujumla kiwango cha kukubalika kwa Rais Magufuli anakubalika na asilimia
96 ya wananchi. Kiwango hiki kinaendana na viwango vya kukubalika kwa
marais wa Tanzania waliopita. Pamoja na hayo, asilimia 88 ya wananchi
wana imani kuwa Rais Magufuli ataendelea na kasi aliyoanza nayo, mpaka
mwisho wa awamu yake ya uongozi”
Aidha
wananchi pia wameonesha viwango vya kukubalika kwa viongozi wao wa
kijiji na serikali za mitaa ambapo wenyeviti na watendaji wa vijini
wanakubalika kwa asilimia 78, diwani kwa asilimia 74 na mbunge kwa
asilimia 68.
Matokeo
haya yametolewa na Twaweza kwenye utafiti uitwao "Rais wa Watu.
Tathmini na matarajio ya wananchi kwa serikali ya awamu ya tano".
Muhtasari huo umetokana na takwimu kutoka Sauti za Wananchi, ambapo wahojiwa 1,813 kutoka maeneo yote Tanzania Bara kati ya tarehe 4 Juni na tarehe 20 Juni 2016 walihojiwa.
Muhtasari huo umetokana na takwimu kutoka Sauti za Wananchi, ambapo wahojiwa 1,813 kutoka maeneo yote Tanzania Bara kati ya tarehe 4 Juni na tarehe 20 Juni 2016 walihojiwa.
Aidha
Wananchi wengi wanasema serikali ya awamu ya tano imeleta maboresho
kwenye huduma nyingi za umma, huku Mamlaka ya Mapato Tanzania ikiongoza
kwa asilimia 85 .
Wananchi
pia wamesema huduma ni nzuri mashuleni kwa asilimia 75, vituo vya
polisi kwa asilimia 74, mahakamani kwa asilimia 73, vituo vya afya
asilimia 72 na mamlaka za maji asilimia 67.
Pamoja
na kiwango kikubwa cha kukubalika kwa serikali ya awamu ya tano na Rais
John Pombe Magufuli, wananchi wapo makini na kanuni za demokrasia na
haki na wanataka zifuatwe.
Wananchi nane kati ya kumi (au 80%) wanasema watendaji wa umma waondolewe pale tu panapokuwepo udhibitisho wa vitendo viovu.
Asilimia
75 wanasema kuwa watendaji waondolewe pale wanaposhindwa kufanya kazi
zao na siyo wanaposhindwa kufuata maagizo ya Rais.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini