Katika
 harakati za kuhakikisha kuwa Mapato yote stahiki yanakusanywa ipasavyo 
na kwa Wakati, Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imejiwekea mikakati 
mbalimbali ya kuongeza wigo wa vyanzo vya Mapato pamoja na kukusanya 
Mapato kikamilifu.
Mikakati hiyo ni kama ifuatavyo;
Kulifanya
 eneo la Kariakoo kuwa Mkoa Maalumu wa Kodi kutokana na eneo hilo kuwa 
kitovu cha biashara hapa nchini na kuhakikisha kila mfanyabiashara 
anakuwa na Mashine ya Kielektroniki ya kodi (EFDs) na kuitumia ipasavyo.
Katika
 kutekeleza hilo Mawakala wote wa EFDs wamefungua ofisi ya pamoja katika
 jengo la Al-Falah Towers lililopo mtaa wa Msimbazi Kariakoo ili 
kurahisisha upatikanaji wa mashine hizo na kutatua changamoto 
zinazowakabili wafanyabiashara katika matumizi ya mashine hizo.
Aidha
 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA Bw. Richard Kayombo 
ametoa wito kwa wananachi na wafanyabiashara kujitokeza kuhakiki taarifa
 zao za usajili wa TIN kabla ya Tarehe 15 Oktoba 2016 katika vituo 
vifuatavyo kwaajili ya zoezi hilo kwani muda hautaongezwa baada ya 
tarehe hiyo maana baada ya tarehe hiyo zoezi hili litahamia mikoa 
mingine;
Vituo hivyo vya uhakiki ni pamoja na:
- Mkoa wa Kodi Ilala: Jengo la Mariam Tower (Shaurimoyo) na 14Rays (Kariakoo-Gerezani)
 - Mkoa wa Kodi Kinondoni: Jengo la LAPF (Kijitonyama) na Kibo Complex (Tegeta) na ofisi za TRA Kimara
 - Mkoa wa Kodi Temeke: Uwanja wa Taifa na Ofisi za TRA Mbagala- Zakiemu
 - Wilaya ya Kigamboni – Ofisi za TRA Kigamboni
 
Pamoja
 na kuhakiki taarifa zao, wafanyabiashara wote ambao hawana TIN nchini 
wanaombwa kufika katika ofisi ya TRA iliyoko karibu nao ili kujisajili 
kuepuka kukumbwa na msako unaondelea hivi sasa nchi nzima pamoja na 
uhamasishaji
Wakati
 huo huo Bw. Kayombo amewahimiza wamiliki wa vituo vya mafuta kutekeleza
 agizo la Serikali la kufunga mashine za EFDs kabla au ifikapo tarehe 30
 Septemba 2016 kwani kinyume na hapo ukaguzi utaanza kufanyika kuanzia 
tarehe 1 oktoba na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote 
watakaobainika kukiuka agizo hilo.
Katika
 kuhakikisha kwamba kodi ya ongezeko la thamani VAT inakusanyawa kwa 
Wakati Mamlaka inawakumbusha walipakodi wote waliosajiliwa na Kodi ya 
Ongezeko la Thamani -VAT kuwasilisha ritani ya kila mwezi kabla au 
tarehe 20 ya kila mwezi badala ya tarehe 27 iliyokuwepo kabla ya mwaka 
hu wa fedha.
Kwa
 upande wa walipa kodi zaa makadirio na kodi za makampuni (Corpoaration 
Tax) wanakumbushwa kulipa kodi zao mapema mwezi hu wa tisa badala ya 
kusubiri msongamano mwisho wa mwezi ambao unaweza kuwasababishia 
usumbufu
Hivyo
 hivyo walipakodi wote wanaodaiwa madeni ya kodi za nyuma au malimbikizo
 wanakumbushwa kutembelea Mameneja wa mikoa, Wilaya na ofisi mbali mabli
 za TRA zinazowahudumia ili kujadiliana namna ya kulipa madeni hayo.
Kutokana
 na mikakti mizuri iliyowekwa na uiongozi wa TRA na serikali Mpaka sasa 
baadhi ya mikakati hiyo imeanza kuonyesha mafanikio na mwelekeo mzuri wa
 makusanyo ambapo kwa kipindi cha mwezi Agosti 2016 TRA imekusanya 
Trillioni 1.158 ikilinganishwa na lengo la Trillion 1.152 ambayo ni 
asilimia 100.57  ambapo Mwezi Agosti Mwaka 2015 TRA ilikusanya Billion 
923.
Wito
 wetu kwa wanahabari na wananchi kwa ujumla ni kuendelea kutuunga mkono 
kwa kuhimiza kutoa risiti pamoja na kudai risiti katika kila manunuzi 
pamoja na kutoa taarifa za dalili za ukwepaji wa kodi wa aina yoyote 
mahali popote nchini
‘Pamoja Tunajenga Taifa Letu’
Richard Kayombo
MKURUGENZI WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI
 Download Video and Put Comment
 Toa Maoni Hapa Chini
