Watu
 watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wanadaiwa kukamatwa na polisi 
wakiwa na zana mbalimbali ambazo hutumiwa na vyombo vya ulinzi zikiwamo 
silaha za vita na sare za polisi.
Vitu
 hivyo vinadaiwa kutumiwa na watu hao kufanya   ujambazi.Inadaiwa kwamba
 watu hao ni wale waliovamia na kuiba fedha katika jengo la Sophia House
 lililopo Keko   Dar es Salam wakiwa wamevaa sare za polisi na kutumia 
gari   ya Noah.
Taarifa 
 kutoka chanzo cha kuaminika zinaeleza kwamba watu hao ni pamoja na 
mwanamke mmoja aliyekamatiwa   Bunju  katika Manispaa ya Kinondoni 
ambako vilikutwa vitu vyote vilivyoporwa na wanaume wawili 
waliokamatiwa   Mbagala Manispaa ya Temeke,   Dar es Salaam.
Chanzo
 hicho kilieleza kwamba silaha zilizokamatwa  ni pamoja na bunduki tatu 
za SMG na risasi zake 260, bastola 16 na risasi zake 526, panga moja na 
michimbiko mitatu ya kung’olea mageti..
Vitu
 vingine ni   pingu za chuma 45 na tatu za plastiki, ‘radio call’  12 , 
kamera ya CCTV moja, gari moja   ya Noah, sare ya polisi jozi moja, 
‘pump action tatu na mkasi mmoja.
 Download Video and Put Comment
 Toa Maoni Hapa Chini
