
Wakiongea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji chao
cha Kachele wilayani Kalambo, wananchi hao wamesema wamejikuta
wakitapeliwa na kudhulumiwa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu, na
hatimaye ardhi yao kuishia mikononi mwa mtu anayejiita mwekezaji kutoka
mkoani Arusha,
na wao kukosa kabisa maeneo ya kilimo huku baadhi ya wanaume wakiuza maeneo yao bila ya kushirikisha familia zao.
Mkuu wa wilaya hiyo ya Kalambo Bw. Wailman Ndile, akiongea na
wananchi hao wa kijiji cha Kachele amemuagiza mwekezaji huyo aliyenunua
shamba hilo lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 1,700, afike ofisini kwake
akiwa na watu wote waliomuuzia eneo hilo, na pia akiwa na muhtasari wa
mkutano mkuu wa kijiji ulioidhinisha kununua eneo hilo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini