
Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi ametoa kauli hiyo mjini Lindi
wakati wa hafla ya kupokea tuzo ya kimataifa ya mazingira aliyoshinda
mkurugenzi wa taasisi ya uhifadhi ya mpingo, Makala Jasper Jijini London
na kukabidhiwa na binti wa malkia wa uingereza, shindano lililokuwa na
washindani zaidi ya 130 kutoka nchi mbalimbali duniani ambapo makala
ameshinda tuzo hiyo kutokana na kazi kubwa anayoifanya katika kuongoza
taasisi ya mpingo kwenye usimamizi wa mazingira na maendeleo endelevu ya
wananchi na jamii.
Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa wilaya za mkoa wa Lindi pamoja
na wananchi wamesema tuzo hiyo inayotolewa na mfuko wa kimataifa wa
uhifadhi wa Whitley wenye makao yake makuu nchini Uingereza yenye hadhi
ya juu duniani ambayo ni ya kwanza kutolewa kwa nchi za afrika itakuwa
kichocheo kwa vijiji vya mkoa wa Lindi kuongeza kasi ya uhifadhi na
kutilia mkazo uvunaji endelevu wa misitu ya vijiji.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini