
Mamlaka
ya mawasiliano Tanzania TCRA imezima namba za utambulisho wa simu laki
sita na elfu tatu katika kampeni ya kuondoa simu feki sokoni huku
wafanyabiashara wakihangaika kuzihamishia nchi jirani ambako bado
zinatumika ikiwemo Comoro, DRC na Msumbiji.
ITV imetembelea katika maduka mbalimbali yanayouza simu za mkononi
na kujionea umati mkubwa wa wananchi wakinunua simu, ambapo akizungumza
na ITV mmoja wa wafanyabiashara aliyejitambulisha kwa jina Hamisi
Selemani amesema wanunua simu hizo kwa lengo la kuziuza katika nchi hizo
ambako zinauwezo wa kufanya kazi.
Aidha wamiliki wa maduka ya simu za viganjani wamesema baadhi ya
simu hizo ambazo hazina namba tambulishi-imei hazijafungwa na kuitaka
mamlaka ya udhibiti wa mawasiliano nchni kufuzifunga ili kuondoa
usumbufu kwa wateja na wafanyabiashara.
Kwa mujibu wa takwimu za mamlaka ya mawasiliano nchi-TCRA-zaidi ya
simu feki za kiganjani laki sita na 30 zimefungiwa mpaka sasa ambapo na
inakadiliwa Tanzania asilimia 2.6 ya simu zote zilikuwa feki kati ya
watumia simu zaidi ya milioni zaidi ya milioni thelathini na tatu.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini