
Siku
chache kabla ya zoezi la kuzima simu bandia nchini Juni 16 mwaka huu
halijatekelezwa rasmi, mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA imewasisitizia
wananchi wote nchini wanaotaka kununua simu mpya kwanza wahakiki simu
hizo kabla hawajazinunua ili kuwa na uhakika wa kununua simu halisi ama
'feki' kwa vile zoezi hilo liko palepale.
Akizungumza katika mkutano wa kuhitimisha programu ya mwendelezo wa
utoaji elimu kwa umma katika suala la uzimwaji wa simu bandia Juni 16
mwaka huu, Mhandisi wa mamlaka ya mawasiliano nchini Mhandisi Imelda
Salum licha ya kukiri uwepo wa simu bandia kwenye soko la Mawasiliano
lakini amesema suala la kutambua simu bandia ama halisi bado ni
changamoto kwa wananchi wengi.
Kwa upande wake afisa viwango wa shirika la ubora wa viwango nchini
TBS Bw, Safari Fungo amekiri changamoto ya uingizwaji wa simu feki
nchini linafanana na la madawa ya kulevya kwavile njia nyingi za panya
hutumika lakini amesema kama TBS watahakikisha ukaguzi wa mara kwa mara
unafanyika katika soko.
Awali akizindua mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa simu za
kiganjani mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikiro pamoja na
kuwataka wanaotumia vibaya mitandao ya mawasiliano kuacha kufanya hivyo
kwani hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao aliwashauri wadau wa
mawasiliano na viwango kuhakikisha wanadhibiti njia zote zinazotumika
kuingiza bidhaa feki nchini.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini