Wanaharakati wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wameikosoa bajeti ya mwaka 2016/17 kutokana na kuzifanya Sh50 milioni zilizoahidiwa na Rais John Magufuli kwa kila kijiji, kuwa za mkopo badala ya kutolewa kama ruzuku.
Katika
tamko lao, wanaharakati hao walisema Serikali itafute vyanzo vingine
vya mapato ili iweze kutoa ruzuku kwa vikundi vya wanawake kwani walio
wengi tayari wana mikopo wliyopewa na taasisi za fedha na hivyo wana
mzigo wa madeni.
Akisoma
tamko hilo, Janeth Mawinza alisema wanawake wana madeni mengi ambayo
wameshindwa kulipa kwa sababu ya kukosa elimu ya kufanya biashara.
“Tuwape
unafuu sasa kwa kuwapa ruzuku, vinginevyo tutawasababishia msongo wa
mawazo kwa kudaiwa na taasisi mbalimbali za fedha,” alisema.
Alisema mpango huo wa mikopo bila kuwapa elimu ya biashara unaweza kusababisha vifo kwa baadhi yao.
Alisema mpango huo wa mikopo bila kuwapa elimu ya biashara unaweza kusababisha vifo kwa baadhi yao.
“Tumeshuhudia
wanawake wananyang’anywa samani zao na kusababisha msongo wa mawazo kwa
sababu ya kukosa elimu ya biashara, tutawaua,” alisema.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini