Leo tutaeleza machache kwa mfano
mtu anaweza kupatwa na kitu kinachoitwa kitaalam Subarachnoid
Haemorrhage, ambapo mpasuko wa mshipa wa damu hufanyika karibu na eneo
linalozunguka ubongo linaloitwa Subarachnoid na mtu kupata kiharusi.
Wakati fulani, mishipa ya damu
huzungukwa na aina fulani za mafuta yasiyofaa mwilini, hali inayoitwa
kitaalam Atherosclerotic plaque. Hali hii husababisha kuganda kwa damu
katika mishipa Thrombosis hiyo.
Kuganda huku kwa damu kunaweza kutokea kwenye mishipa mikubwa au midogo inayopeleka damu kwenye ubongo.
Baadhi ya mishipa mikubwa ya damu
inayoweza kuathirika na tatizo hili ni pamoja na Arteri za Common
Carotid na Interior Carotid Arteries na Arteri za Vertebral. Nyingine ni
mishipa midogo inayounda eneo linaloitwa Circle of Willis lililo katika
ubongo, hivyo mgonjwa kujikuta akikumbwa na kiharusi.
Kuganda kwa chembe nyekundu za damu za
mgonjwa wa Sickle Cell kunaweza pia kusababisha kuziba mishipa ya damu
hivyo kusababisha kiharusi.
Kuganda kwa damu kwenye mishipa ya damu
ya sehemu nyingine za mwili au (hewa, mafuta, kusanyiko la vijimelea
kama bakteria waletao ugonjwa wa Endocarditis) huweza kusababisha kuziba
kwa mishipa inayosambaza damu kwenye ubongo na hivyo kusababisha
kiharusi.
Upungufu wa usafirishaji damu mwilini
Systemic Hypoperfusion – Wakati fulani moyo hushindwa kusukuma damu
vizuri kwenda sehemu mbalimbali za mwili, ikiwemo ubongo kutokana na
kufa kwa sehemu za nyama ya moyo kwa kukosa damu ya kutosha Ischaemic
Heart Diseases au kutokana na kujaa kwa maji kwenye gamba lake la nje au
kupungua kwa damu mwilini, kunakoweza kusababishwa na mambo kadhaa.
Hali hii husababisha sehemu kubwa ya
mwili ikiwemo ubongo kukosa oksijeni ya kutosha na kusababisha
kuathiriwa kwa sehemu ya ubongo.
Shinikizo la damu la muda mrefu
lisilodhibitiwa linaweza kusababisha kupasuka kwa mishipa midogo
inayosambaza damu kwenye ubongo na hivyo damu kujaa kwenye ubongo na
mgonjwa kukumbwa na kiharusi.
Dalili za kiharusi
Dalili za kiharusi hutegemea na eneo la
ubongo lililoathiriwa. Iwapo sehemu ya ubongo mkubwa Cerebellum
itaathirika, mgonjwa atakuwa na dalili za wazi kama vile kushindwa
kutembea vizuri, hivyo kuathiri mwendo wake, kujihisi kizunguzungu na
pia kutapika.
Iwapo sehemu ya ubongo wa kati Cerebral
Cortex itakuwa imeathirika, mgonjwa atakuwa na dalili za kushindwa
kuongea, kushindwa kuelewa lugha inayozungumzwa, kushindwa kuona vizuri,
kuwa na ukosefu wa kumbukumbu, kuwa na mvurugiko wa mpangilio wa
kufikiri na kuchanganyikiwa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini