Yanga yamsainisha Twite yamtema Issoufou Boubacar. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Tuesday, June 7, 2016

Yanga yamsainisha Twite yamtema Issoufou Boubacar.



Kiungo Mniger Issoufou Boubacar kulia akiwa na Mkuu wa kitengo cha habari na mahusiano cha Klabu ya Yanga Jerry Muro
Garba ameachwa kwa sababu ya kushindwa kuwa katika kiwango kinachohitajika kwa matumizi ya timu hiyo, wakati Mbuyu kwa mara nyingine akijivunia matunda ya kazi yake awapo uwanjani.
Garba alisajiliwa na Yanga SC Desemba mwaka jana baada ya majaribio ya siku mbili tu, lakini tangu hapo amecheza mechi 11 na kufunga mabao matatu likiwemo lile la katika sare ya 1-1 na Al Ahly ya Misri mjini Dar es Salaam katika Ligi ya Mabingwa Afrika miezi miwili iliyopita.
Kabla ya kutua Klabu ya Yanga Garba amewahi kuchezea AS FAN na AS Douanes zote za kwao Niger, Muangthong United na Phuket za Thailand, Club Africain na ES Hammam-Sousse za Tunisia.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin