Licha
ya wananchi wanaovamia migodi kwa lengo la kuiba madini hapa nchini
kuendelea kupoteza maisha bado tatizo hilo limekuwa sugu kwa wananci
wanaouzunguka mgodi wa geita huku uongozi wa migodi hiyo ukiendelea
kuomba serikali kuongeza jitihada za kusaidia kuwaelimisha wananchi hao
ili watambue madhara ya kuvamia migodi.
Akizunguza na ITV Mkurugenzi mtendaji wa mgodi huo amesema tatizo
la wavamizi kwenye mashimo ya migodi limekuwa sgu huku wengi wa wananchi
wanafanya vitendo hivyo wakiendelea kupoteza maisha ambapo amesema
licha ya kufanya vikao na uongozi wa kijiji bado haijasaidia na kuomba
serikali kuu kuona nini cha kufanya.
Meneja wa uchimbaji wa madini katika migodi ya geita Bwana.
Ndibalema Alistides amesema licha ya mgodi huo kutoa ajira kwa vijana
wengi wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo bado baadhi yao wamekuwa
wakiendelea kuvamia licha ya mazingira kutokuwa rafiki na kutoa wito kwa
wanachi kuacha mara moja tabia hiyo hatarishi.
Nao baadhi ya wanachi wanaovamia migodi hiyo licha ya kubaini
kufahamu madhara ya kuvamia mashimo ya migodi hiyo wamesema wamekuwa
wakifanya hivyo kutokana na hali ngumu ya maisha na kutoa wito kwa
uongozi wa migodi na serikali.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini