Wananchi
wa wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi wameshindwa kuvuka upande
mmoja kwenda mwingine baada ya kukatika kwa daraja linalounganisha
barabara ya kutoka Morogoro kwenda maeneo hayo, katika eneo la Mang'ula A
wilayani Kilombero, jambo lililosababisha adha kubwa kwa wasafiri
wanaotumia barabara hiyo.
Hali hiyo imejitokeza baada ya kunyesha kwa mvua kubwa hali
iliyosababisha wasafiri na watumiaji wengine wa barabara hiyo kushindwa
kuvuka upande mmoja kwenda mwingine ambapo baadhi ya wananchi wamesema
daraja hilo limekatika kutokana na uchakavu kutokana na kujengwa kwa
muda mrefu, na limekuwa likipitidha mizigo yenye uzito mkubwa na kwamba
mara kwa mara maeneo hayo yamekuwa na kero sugu ya kukatika kwa
mawasiliano kutokana na uharibifu wa miundombinu ya barabara bila
kupatikana suluhisho la kudumu.
Wasafiri walio kwama katika eneo hilo wameeleza kusikitishwa na
hali hiyo kwani wamekwisha toa taarifa mapema kwani walitoa taarifa kwa
mamlaka mbalimbali bila mafanikio na kwamba madhumuni yao ya kibiashara
na shughuli binafsi yamejikuta yĆ kikwama na kutumia fedha za matumizi
mengine kujikimu na kusababisha hasara.
Msemo wa kufa kufaana ulidhiirika pale ambapo wafanyabiashara za
vyakula na wasafirishaji wa abiria kwa kutumia pikipiki maarufu kama
bodaboda waliipoonekana kufurahia hali hiyo kwa madai imewawezesha
kujipatia kipato kibwa hivyo kuomba hali hilo kuendelea ili kupata
fedha.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini