Mahakama
ya hakimu mkazi Kisutu Dar es Salaam inatarajia kutoa maamuzi ya
kupatiwa ama kunyimwa dhamana kwa watumiwa watatu akiwemo aliyekuwa
kamishina mkuu wa TRA wanaokabiliwa na makosa manne likiwemo la
utakatishaji wa fedha mapema April 22 mwaka huu.
Hati ya mashitaka inawataja watuhumiwa wote watatu kila mmoja
akikabiliwa na mashitaka manne, huku mshitakiwa wa pili aliyewahi
kushika taji la Miss Tanzania mwaka 1996 akikabiliwa na mashitaka
mawili zaidi.
Wanasheria kutoka upande wa utetezi walikuwa na kazi moja ya
kutumia vifungu vya sheria hasa sheria ya utakatishaji fedha, ili kuona
namna wanavyoweza kuwanasua watuhumiwa hao kwa dhamana.
Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo Emilius Mchauru, jopo la
utetezi kwa watuhumiwa hao likiongozwa Dkt Ringo Tenga, walipinga
shitaka namba 8 la utakatishaji wa fedha amablo liliawsishwa na upande
wa serikali kwa kutumia kifungu namba 12 A, na kuiomba mahakama kuruhusu
kifungu hicho kusomwa kuanzia A hadi D, tofauti ilivyowasilishwa na
mahakama.
Hata hivyo upande wa serikali kupitia kwa wakili wa mwanasheria
mkuu wa seriakli Oswad, uliendelea kubaki na msimamo wake wa kusoma
kifungu namba 12 A, pekee, jambo lililozua mvutano mkali wa kisheria, na
hatimaye hakimu Mchauru akaiahirisha kesi hiyo hadi April 22 mwaka huu
ili kutoa uamuzi kuhusu dhamana za watuhumiwa hao.
Katika shitaka la nane watuhumiwa hao wanakabiliwa na tuhuma za
utakatishaji wa fedha kiasi cha Dola za Marekani 6 milioni, shitaka
ambalo kisheria halina dhamana ambapo watuhumiwa wote wamerejeshwa
lumande hadi april 22 mwaka huu.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini