Mmoja
wa vijana ambaye anasadikiwa ndiye aliyekuwa kinara wa kuhamasisha
maandamano ya wanafunzi wa vyuo vya Mtakatifu Joseph vya Tawi la Songea
vilivyofungwa na serikali akiwa chini ya ulinzi wa kikosi cha kuzuia
fujo FFU kutokana na kufanya maandamano kinyume cha utaratibu wakitaka
kwenda kumuona Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi wakati
walipodhibitiwa maeneo ya shule ya Bunge posta wakielekea wizarani leo.
TUME
ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ilifuta kibali kilichoanzisha vyuo vikuu
viwili vishiriki vya Mtakatifu Joseph ambavyo ni Chuo Kikuu kishiriki
cha Sayansi ya Kilimo na Teknolojia (SJUCAST) na Chuo Kikuu kishiriki
cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (SJUIT) vilivyopo Songea.
Baadhi
ya askari wakijiandaa kuzuia maandamano ya wanafunzi hao leo maeneo ya
wizara ya Fedha na Mipango Posta jijini Dar es salaam.
Wanafunzi
hao wakifurumushwa na polisi mara baada ya kuktwa wakiandamana bila
kibali kwenda kumuona Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini